Η παρουσίαση φορτώνεται. Παρακαλείστε να περιμένετε

Η παρουσίαση φορτώνεται. Παρακαλείστε να περιμένετε

KI 107: UTANGULIZI WA MISINGI YA ISIMU

Παρόμοιες παρουσιάσεις


Παρουσίαση με θέμα: "KI 107: UTANGULIZI WA MISINGI YA ISIMU"— Μεταγράφημα παρουσίασης:

1 KI 107: UTANGULIZI WA MISINGI YA ISIMU

2 Fonetiki na Sauti za Lugha
Fonetiki ni nini? Asili ya neno hili ni neno la kigiriki “phonetica” ambalo limeundwa na maneno mawili “phone” (sauti) na “tica” (uchunguzi).

3 Fonetiki Mgullu (1999:20), Massamba na wenzake (2004:5) na Besha (1994:18) wanaeleza kuwa Fonetiki hushughulikia uchambuzi na uchunguzi wa taratibu zote zinazohusiana na utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za mwanadamu. Hyman (1975) fonetiki ni taaluma ambayo hususani huchunguza sauti ambazo hutumiwa na wanadamu wakati wanapowasiliana kwa kutumia lugha.

4 Uchunguzi wa kifonetiki hauhusishwi na lugha yoyote maalum.
Kipashio ambacho hutumiwa katika uchambuzi wa kifonetiki ni foni. Hyman anasema foni ni kipande kidogo kabisa cha sauti kisichohusishwa na lugha yoyote. Kwa hiyo foni ni istilahi ambayo hutumiwa kuelezea sauti za lugha ambazo hazimo kwenye lugha yoyote mahsusi. Foni ni kipashio cha kifonetiki na sio cha kifonolojia.

5 fonetiki Kipacha, A. (2007) anasema fonetiki ni taaluma ya uchambuzi wa sauti za lugha. Anasema kietimolojia fonetiki imebeba dhana mbili (i) foni na (ii) etiki. Foni maana yake ni sauti Dhana ya etiki ni uchambuzi wa tofauti za sauti katika hatua ya awali ya ukusanyaji data.

6 fonetiki Fonetiki ni taaluma ya isimu inayochunguza (sauti zote zinazotamkwa na binadamu ambazo hazihusishwi na lugha maalum) na kipashio chake ni ‘foni’. Fonetiki hushughulikia uchambuzi na uchunguzi wa taratibu zote zinazohusiana na utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za mwanadamu.

7 ... Dhima ya fonetiki ni kuchunguza maumbo mbali2 ya sauti zinazoweza kutolewa, kusafirishwa, kumfikia msikilizaji, kufasiliwa na ubongo; bila kujali sauti hizo zinatumika katika lugha gani.

8 Fonetiki huchunguza: kuainishwa
i. Jinsi sauti inavyotamkwa, pambanuliwa na kuainishwa ii. Jinsi sauti zinavyosafiri kutoka kwa mtamkaji hadi kwa msikilizaji iii.Jinsi sauti zinavyofasilishwa kwa kutumia sikio kupitia neva za masikizi hadi ubongoni.

9 Matawi ya Fonetiki i. Fonetiki Matamshi (articulatory phonetics)
Huchunguza jinsi sauti za lugha zinavyotolewa na ala sauti za binadamu ii. Fonetiki akustika au fonetiki mawimbi sauti Huchunguza jinsi mawimbi sauti yanavyoweza kusafiri kutoka kinywa cha msemaji hadi sikio la msikilizaji.

10 iv. Fonetiki tiba matamshi (tawi jipya)
Matawi ya fonetiki iii. Fonetiki masikizi (auditory phonetic) Hujishughulisha na uchunguzi na uchanganuzi wa namna sauti za lugha zinavyokamatwa na sikio zikasafirishwa kwenda katika ubongo kupitia neva zinazohusika katika utamkaji. iv. Fonetiki tiba matamshi (tawi jipya) Tawi hili hujihusisha na matatizo yanayoambatana na utamkaji wa sauti na jinsi ya kuyatatua. Mfano kushindwa kutofautisha sauti moja na nyingine mfano: /l/ na /r/, /p/ na /b/ au tatizo la kithembe.

11 Fonetiki Matamshi i. Ala za sauti/matamshi na mikondo hewa.
Sauti za lugha ya mwanadamu hutamkwa pale ambapo viungo mbalimbali vya mwili wa binadamu hukatiza hewa inayoingia na kutoka mapafuni kupitia ama chemba ya pua au chemba ya kinywa. Viungo hivi vya mwili wa binadamu huitwa ala za sauti.

12 ... Kuna aina 2 za ala za Sauti/Matamshi.
Ala tuli (viungo visivyosogea) passive speech organs Ala sogezi (viungo vinavyosogea) active speech organs

13 ... Ala tuli: ni viungo visivyobadilisha mahala pake pa kawaida ktk mchakato wa utamkaji kama vile: ufizi, kaakaa gumu, kaakaa lani, meno n.k. Ala sogezi: ni viungo vya mwili vinavyosogeasogea wakati wa utamkaji wa sauti za lugha mfano ulimi, midomo, kidakatonge. MUHIMU: Ala za sauti ni vile viungo vyote vinavyoshiriki katika utoaji/utamkaji wa sauti za lugha zisemwazo na binadamu.

14 Mkondo hewa Njia ambayo hewa hupitia ama kutoka mapafuni kwenda nje au kutoka nje kwenda mapafuni (Massamba, 2004). Mkondo hewa ambao husukumwa nje ya bomba la sauti, huitwa mkondo hewa- nje na ule uingiao ndani huitwa mkondo hewa- ndani. Takriban sauti zote za lugha ya mwanadamu hutamkwa kwa kutumia mkondo hewa nje.

15 Mkondo hewa... Kuna sauti chache sana ktk baadhi ya lugha hutamkwa kwa mkondo hewa –ndani mfano: vidoko ktk lugha ya Kikhosa na Kizulu Aina hizi za sauti hutamkwa kwa hewa kuvutwa ndani kwa haraka na kisha husukumwa nje kwa vipimo huku ikiathiriwa na ala sauti na hivyo kusababisha aina mbalimbali za sauti za lugha.

16 Aina za Sauti kwa mujibu wa Alfabeti ya kifonetiki ya Kimataifa na utamkaji wake.
Uainishaji wa sauti Sauti za lugha zimegawanyika katika makundi makubwa mawili: konsonanti na irabu. Tofauti kati ya konsonanti na irabu ipo katika utamkaji wake. Wakati wa kutamka irabu hewa haizuiwi au kubanwa mahali popote, yaani hewa kupita kwa urahisi bila kuzuiwa na wakati wa kutamka konsonanti hewa huzuiwa au kubanwa kutokana na msogeano wa ala za sauti.

17 Sauti za Irabu Uainishaji wa Irabu Irabu ziko nyingi na kila lugha inayo idadi tofauti. Lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa lugha ambazo zinatumia irabu chache sana katika mfumo wake wa sauti. Lugha hii ina irabu 5. Lugha zilizo nyingi zina irabu zaidi ya tano. Tunapoainisha irabu, tunaangalia sifa za irabu hizo wakati wa utamkaji.

18 Mambo/Vigezo vya kuzingatia utamkaji irabu
i. Mwinuko ulimi wakati wa utamkaji. ii. Mkao wa mdomo wakati wa utamkaji iii. Mahali pa kutamkia

19 Utamkaji wa Irabu i. Mwinuko ulimi katika kinywa wakati wa utamkaji.
Kinachoangaliwa wakati wa utamkaji wa irabu hizo ni ulimi kama umeinuka: juu sambamba na paa la kinywa, umeinuka kiasi au upo chini sambamba na sakafu la kinywa.

20 Kutamka irabu... Kama irabu inatamkwa ulimi ukiwa umeinuliwa juu sambamba na paa la kinywa basi irabu hiyo huitwa ni irabu ya juu na kama irabu inatamkwa ulimi ukiwa umeinuliwa kiasi huitwa irabu za nusu juu na nusu chini na kama irabu inatamkwa ulimi ukiwa umelala chini basi irabu hiyo huitwa ni irabu ya chini.

21 Kutamka irabu si rahisi sana kuweka mipaka kati ya vokali za nusu juu na nusu chini. Mifano ya aina za irabu ktk lugha ya Kiswahili kwa kuzingatia kigezo ni: Irabu za juu ni /i/ na /u/ na za nusu juu ni /o/ na /e/ , nusu chini ni /ε / na /ᴐ/ na ya chini ni /a/.

22 Vigezo... ii. Mkao wa mdomo wakati wa utamkaji
wakati wa kutamka irabu fulani mdomo unakuwa wa mviringo au umekaa bapa/tandazwa. Irabu zinazo tamkwa mdomo ukiwa umeviringwa huitwa irabu viringe na zile zinazotamkwa mdomo ukiwa umetandazwa huitwa irabu mtandazo. Tafiti zilizofanyika hivi karibuni zinaonyesha kuwa irabu zote za nyuma ni irabu mviringo na zile za mbele ni irabu mtandazo au bapa.

23 ... iii. Mahali pa kutamkia. Hapa tunaangalia sehemu ya ulimi inayohusika wakati wa kutamka irabu. Sehemu za ulimi zinazohusika na utamkaji wa irabu zimegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni: sehemu ya mbele katika bapa pamoja na ncha ya ulimi sambamba na ufizi na meno, sehemu ya kati ni kiwiliwili cha ulimi sambamba na kaakaa gumu na sehemu ya nyuma ya ulimi ni shina.

24 Sauti inayotamkiwa... mbele ya ulimi huitwa sauti ya mbele mfano /i/, /e/ na /ε /, inayotamkiwa kati huitwa ya kati mfano /a/ na inayotamkiwa nyuma huitwa irabu ya nyuma mfano /u/, /o/ na na /ᴐ/.

25 ... Kutokana na taaluma ya fonetiki irabu ziko nyingi sana na kila lugha inayo idadi tofauti. Lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa lugha ambazo hutumia irabu chache sana katika mfumo sauti wake, yaani ziko irabu tano. Lugha zilizo nyingi zina irabu zaidi ya tano kwa mfano kuna lugha zina irabu saba, nyingine irabu tisa n.k.

26 ... Wanafonetiki huziwakilisha irabu hizi kwa namna tofauti kwa kila lugha ili kuonesha tofauti na uhusiano uliopo baina yao. Hata hivyo kuna makubaliano ya kutosha kuwa irabu za msingi ziko nane ambazo ni:

27 ... Mbele Nyuma

28 Irabu za Kiswahili sanifu
Mbele Nyuma

29 ... Katika taaluma ya isimu irabu hizi zimepewa sifa maalum za kuzibainisha, Sifa hizo ni kama ifuatavyo ni safa bainifu.

30 Nduni Bainifu za Irabu za Kiswahili sanifu

31 Uainishaji wa Konsonanti
Uainishaji wa sauti konsonanti huzingatia mambo makuu matatu ambayo ni: i. Mahali pa matamshi (ala sauti), ii. Namna au jinsi ya matamshi iii. Hali ya nyuzi sauti.

32 Sauti za Lugha ya Kiswahili kwa mujibu wa IPA
Ghuna/sighu Mid meno Ufizi Kaakaa gumu Kaa kaa laini Glota Vipasuo b/p d/t g/ k Vipasuo Kwamizi Ɉ au ǰ ʧ au č Vikwamizi f/ v ð/ θ z/s ɤ h Vitambaza l Vimadende r Nazali Viyeyusho m w n ɲ y ŋ

33 1. Mahali pa matamshi/Ala za sauti
Mahali pa kutamkia: hapa kinachoangaliwa ni konsonanti imetamkiwa wapi: midomo, midomo- meno, ufizi, kaakaa gumu, kaakaa laini, glota. Kwa mfano: /p/ ni konsonanti ya midomo. Hebu tujikumbushe kidogo aina za konsonanti kwa kuangalia sifa hii:

34 ... Midomo Meno Ufizi Kaakaa gumu Kaakaa laini Koromeo au glota Ulimi

35 2. Namna au jinsi ya matamshi
Hali ya mkondo hewa-wakati wa utamkaji mkondo hewa huweza: kuzuwiwa moja kwa moja, kuzuwiwa moja kwa moja na kuachiwa ghafla, kuzuwiwa kidogo na kuachiwa ghafla, hewa kutoka kwa kukwamakwama nk Hapa tunapata aina mbalimbali za konsonanti. Aina hizo ni kama zifuatazo: vipasuo-huitwa pia vizuio/vizuwiwa, vipasuo kwamizi, vikwamizi, nazali, kitambaza, kimadende na kiyeyusho.

36 ... a. Vipasuo/vizuio Hizi ni sauti konsonanti ambazo wakati wa utamkaji wake, hewa kutoka mapafuni kupatia chemba ya mdomo hubanwa kabisa na kisha kuachiwa ghafla. Hali hii husababisha utokeaji wa sauti mfano wa mlipuko. Mfano wa sauti hizi ni [p],[b],[t],[d],[k],[g]

37 ... b. Vipasuo kwamizi/vizuiwa kwamizwa
Wakati wa kutamka sauti hizi hewa kutoka mapafuni huzuiwa na kuachiwa kwa kukwamizwa kwamizwa katika kaakaa gumu sauti hizo ni [ʧ] na [Ɉ].

38 ... c. Vikwamizi: Sauti hizi hutamkwa pale ambapo ala za matamshi huwa zimekaribiana kiasi kwamba hewa kutoka mapafuni inapopita katikati ya ala hizi mkwaruzo husikika. Vikwamizi katika lugha ya Kiswahili ni [f], [v], [ð], [s],[z], [ʃ], [x],[ɤ], na [h]

39 ... d. Vilainisho Ni kitamkwa kifulizwa ambacho hutamkwa kwa kutumia ncha ya ulimi na ufizi kwa kutandaza ulimi na kupitisha hewa pembeni. Katika lugha ya Kiswahili kuna vilainisho viwili: i. Kimadende: Hutamkwa ncha ya ulimi ikiwa inagongagonga kwa haraka kwenye ufizi na sehemu ya nyuma ya ulimi imegusa uvula/kimeo. -Kipo kimoja tu [r]

40 ... ii. Kitambaza: Hutamkwa wakati ncha ya ulimi inapogusana na ufizi huku sehemu ya kati ya ulimi imegusa kaakaa gumu na kuacha nafasi ndogo ya hewa kupita ikisababisha mkwaruzo mdogo. Katika lg ya Kiswahili kuna kitambaza kimoja [l]

41 (iii) Kigezo cha nyuzi sauti
Kwa kutumia kigezo cha nyuzi sauti tunapata aina mbili za konsonanti ambazo ni ghuna na si ghuna. Sauti ghuna hutamkwa wakati nyuzi sauti zinapokuwa zinatetema. Sauti ghuna hupewa sifa hiyo kwa kuwekewa alama ya [+ghuna] Sauti si ghuna huwekewa alama ya [-ghuna]. Sauti ambazo si ghuna wakati wa kuzitamka nyuzi sauti huwa hazitetemi.


Κατέβασμα ppt "KI 107: UTANGULIZI WA MISINGI YA ISIMU"

Παρόμοιες παρουσιάσεις


Διαφημίσεις Google